MAGONJWA YA MAUNGIO YA MIFUPA
Arthritis ni ugonjwa wa maungio ya mifupa ya binadamu. Ugonjwa huu hutokana na kuwepo kwa tatizo fulani katika maeneo ya maungio ya mifupa. Arthritis ni mkusanyiko wa magonjwa zaidi yanayohusisha maungio ya mifupa. Katika kipengele hiki tutatazama aina chache hivi za magonjwa ya maungio ya mifupa.
OSTEOATHRITIS
Ni ugonjwa wa maungio ya mifupa unaotokea pale cartilage inaposagika na kupoteza ubora wake. Hali hii husababisha mifupa inayokutana kwenye maungio kusagika moja kwa moja na kusababisha maumivu makali ya mifupa. Watu wenye umri mkubwa na wenye unene mkubwa huwa katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya ugonjwa wa maungio ya mifupa. Wanawake ndio hupata ugonjwa huu zaidi kuliko wanaume.
Ugonjwa huu hushambulia zaidi mikono,magoti,nyonga,shingo na upande wa chini wa mgongo.Huambatana na maumivu makali katika joints, joints hukaza hasa unapoamka asubuhi ama baada ya kukaa kwa muda mrefu,shida katika kutembea na wakati mwingine joints huvimba na kuonekana nyekundu na zenye joto unapozigusa. Huanza taratibu lakini maumivu huongezeka kwa kadri muda unavyoongezeka.
RHEUMATOID ARTHRITIS
Aina hii ya ugonjwa wa arthritis hutokea pale kinga za mwili zinaposhambulia maungio ya mifupa. Kuna wakati kinga za mwili hushambulia sehemu fulani ya mwili tatizo linalojulikana kama Autoimmune. Kinga hizi hushambulia utando unaofunika maungio ya mifupa na kusababisha mifupa inayozungukwa na utando huo kusagika na cartilage kupoteza ubora wake kabisa.
Tofauti na osteoarthritis,rheumatoid arthritis huathirimwili wote. Madhara yake hufikia kuathiri mapafu na mfumo mzima wa upumuaji,macho,ngozi,mdomo na tezi ya mate,moyo,damu na mishipa ya damu.
By Dr Salome Ndayabanye
Chapisha Maoni